Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tarjuma cha Shirika la Habari la Hawza, Papa katika hotuba yake alisema: “Ninaonesha mshikamano wangu na watu wote wanaoteseka duniani.”
Katika hotuba yake ya Jumapili, baada ya kusoma dua kuhusiana na yale yaliyotangazwa kutoka Ghaza katika wiki iliyopita, alirejelea picha za watoto waliokonda sana waliokufa kwa sababu ya utapiamlo mkali, mashambulizi ya mabomu kwenye hospitali, kumwagwa damu katika mistari ya maji na chakula, na kufungwa njia za msaada wa chakula kwa watu wa Ghaza waliokufa njaa.
Aidha, alisema kuwa: “Katika hali ambayo watu wa Ghaza wanazama kwenye bahari ya njaa, ukatili na mauti, hali hii imezua wasiwasi wa jumla duniani kote.”
Chanzo: Habari za Vatikan
Maoni yako